Jumamosi , 30th Mar , 2024

Watumishi watano wa kituo cha afya cha Mikanjuni kilichopo jijini Tanga wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi baada ya kufanya uzembe uliosababisha kifo cha mama mjamzito  Fatuma Mussa Suleiman aliyekuwa amelazwa kituoni hapo baada ya kumuwekea damu ambayo hakustahili kupewa.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji taarifa kwa waandishi wa habari

Damu aliyowekewa marehemu ilikuwa ni ya mgonjwa mwingine ambaye alikuwa amelazwa kwenye kituo hicho akipatiwa matibatu, na baada ya kupatiwa damu hiyo alianza kuonesha dalili za mtu mwenye mzio mkali (Allergic reaction)  na hatimaye kufariki. 

Watumishi hao waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi ni pamoja na Fadhila Ally Hozza aliyekuwa zamu ya mchana, Restuta Kasendo Deusdedit,  Muya Ally Mohamed walioingia zamu ya usiku huku madaktari waliomfanyia upasuaji avzoAndrew Eliasikia Kidee na Hamis Mohamed Msanii. 

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Mkoani Tanga Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amesema kuwa mama huyo  alilazwa katika kituo cha afya Mikanjuni tarehe 27.3.2024 saa kumi alfajiri kwa tatizo la uchungu. 

"Mgonjwa alifanyiwa upasuaji ambapo alifanikiwa kupata mtoto wa kike wa kilo 3.4 na hakuwa na changamoto yeyote kwa mama na mtoto baada ya upasuaji aliendelea kupatiwa matibabu baada ya upasuaji chini ya uangalizi wa wauguzi na madaktari wa zamu, "alisema Kaji. 

"Katika wodi aliyokuwa amelazwa marehemu kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa anahitaji kuwekewa damu na damu yake ilikuwa tayari imeandaliwa muuguzi aliyekuwa 

"Katika wodi hiyo alipokuwa amelazwa marehemu kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa anahitaji kuwekewa damu na damu yake ilikuwa tayari imeandaliwa muuguzi aliyekuwa zamu alimuwekea marehemu damu ambayo hakustahili kupewa na hakuwa na uhitaji huo,  baada ya kuwekewa damu marehemu alipatwa na mzio mkali (Allergic reaction)  iliyopelekea kifo chake, "alibainisha Kaji. 

Kaji amesema  baada ya tukio hilo  kamati ya mapitio ya vifo vitokanavyo na uzazi ya Halmashauri ya jiji la Tanga ilikutana kujadili sababu za kifo hicho na ilibaini mapungufu mbalimbali ikiwemo kutokuwepo kwa taarifa ya matibabu anayistahili kupata mgonjwa baada ya kutoka chumba cha upasuaji hivyo mgonjwa alikuwa akipewa matibabu pasipokuwa na maandishi yanayoelekeza anachostahili kupewa. 

Mapungufu mengine ni kutokuwepo kwa makabidhiano ya kimaandishi ya wagonjwa kwenye kitabu cha ripoti na pia makabidhiano ya wagonjwa kitanda kwa kitanda hayakufanyika kwa ufasaha huvyo kusababisha mgonjwa kupewa matibabu yasiyo yake. 

Aliongeza kuwa mapungufu mengine ni muuguzi aliyetoa matibabu kwa marehemu hakuzingatia kama taratibu za utoaji matibabu kwa mgonjwa hivyo kupelekea kutoa matibabu yasiyo sahihi kwa mgonjwa. 

Lakini pia wauguzi waliokuwa zamu hawakutoa taarifa mapema za mabadiliko ya hali ya mgonjwa kwa daktari wa zamu na hata baada ya kuona mgonjwa anaonyesha dalili za mwanzo za mabadiliko ya hali ya mgonjwa kwa daktari wa zamu na hata baada ya kuona mgonjwa anaonyesha dalili za mwanzo za mabadiliko ya hali yake waliendelea kukaa kimya hadi mgonjwa alipozidiwa zaidi. 

Mkuu wa ilaya ya Tanga, James Kaji amesema marehemu ameacha kichanga chake kikiwa na afya njema. 

Hata hivyo Kaji amesema Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya wasaidizi wake wanaofanya kazi bila uadilifu na hawafuati utaratibu.