Jumatano , 22nd Jun , 2016

Wakala wa ukaguzi wa Madini nchini Tanzania (TMAA) umesema kuwa kwa kipindi cha July mwaka 2012 na June 2016 jumla ya kesi 98 zimefunguliwa za utoroshwaji wa madini yenye thamani ya shilingi bil 1.3 na dola za kimarekani milioni 10.8 kwenda nje.

Akiongea na waandishi wa habari Kaimu Mtendaji Mkuu wa TMAA Mhandisi Gilay Shamika amesema kuwa kuna wachimbaji na wafanyabiashara ambao si waaminifu ambao huamua kupeleka madini nje ya Tanzania bila ya kufuata sheria zinazotakiwa.

Aidha amebainisha kuwa katika kesi hizo 98 madini ya Tanzanite yameonekana kutoroshwa zaidi kulikoa aina nyingine ya madini hivyo wakala unaongeza nguvu katika kuhakikisha ulinzi unakuwepo maeneo ya uwanja wa ndege na mipakani kwa ujumla.