Ijumaa , 12th Aug , 2022

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, amewahakikishia wananchi na watanzania kuwa, kesi nyingi zilizokuwa zimekwama kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upelelezi kwa sasa kesi hizo tayari zimekwisha shughulikiwa na mamlaka zinazohusika

IGP  Wambura amesema hadi sasa zipo kesi chache ambazo zipo chini ya upelelezi

IGP Wambura amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa, Wakuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mikoa na Wakuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Mikoa ambapo amesema kuwa, kutokana na ushirikiano uliopo kwenye suala la utendaji na kuwa na mawasiliano ya karibu umesaidia kushughulikia upelelezi wa kesi na uendeshaji wa mashtaka