Damu iliyohifadhiwa
Imeelezwa kuwa idara ya upelelezi nchini humo, imeanzisha uchunguzi kwa ushirikiano na Wizara ya Afya ili kuhakikisha wahusika wa sakata hilo wanachukuliwa hatua za kisheria kwani kitendo hicho kimesababisha madhara katika hospitali za umma.
"Inashangaza sana na ni kinyume cha maadili, damu imekuwa ikiuzwa nje ya mipaka ya Taifa la Kenya, hali ni mbaya, imefikia hatua mama aliyejifungua anatakiwa kuongezewa damu, lakini tukija kuangalia hakuna, tunabaki kujiuliza sisi wenyewe ni kitu gani ambacho tunapaswa kukifanya" amesema Waziri wa Afya wa Kenya.
Waziri wa Afya ameongeza kuwa kati ya Mwaka 2018 na 2019 ni asilimia moja tu ya Wakenya, waliojitokeza kuchangia damu kwa hiari.

