Jumatatu , 26th Sep , 2022

Nchi za Kenya  na Namibia zimepunguza  gharama za mawasiliano ya simu na kuwa nchi mbili ambazo zina gharama nafuu zaidi za kupiga simu katika bara la Afrika. 

Kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu , Namibia  itapunguza gharama za mawasiliano kwa silimia 50 , ambapo kwa mujibu wa  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya mawasiliano nchini Namibia , Emilia Nghikembua amesema kuwa moja ya gharama kubwa za mawasiliano ni kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine , na kwamba punguzo hilo limenuia kuongeza ushindani zaidi.  

Ameongeza kwamba kwa sasa wateja wanaweza wasione tija ya punguzo hilo, lakini tija hiyo itaonekana pale ambapo ushindani utaanza kuwa mkubwa  haswa kwa makampuni ya simu kupunguza viwango vya gharama.

Mamlaka ya mawasiliano nchini  Kenya mwezi uliopita ilipunguza gharama za mawasiliano kutoka  shilingi za Kenya  0.99 (sawa na shilingi za Kitanzania  kufikia  Ksh 0.58 (Tsh. 11.6)

 

 Nigeria na Afrika Kusini na zenyewe zimekua na mipango ya kupunguza gharama za mwasiliano ya simu.