Jumapili , 25th Mei , 2014

Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, linakabiliwa na kuzorota kwa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo miundombinu ya barabara, afya pamoja na elimu, huku idadi kubwa ya vijana katika jimbo hilo wakiwa hawana shughuli za kufanya.

Mvua na mafuriko imekuwa chanzo cha kuharibu miundombinu kama inavyoonekana pichani hapo juu.

Hayo yamebainishwa jana na jumuiya ya wazazi kata ya Kunduchi ambapo katibu wake hiyo Bi. Suzan Bakari ametaja sababu ya kuwepo kwa hali hiyo ni kutokana na jimbo hilo kushikiliwa na chama cha upinzani ambacho amedai kimeshindwa kutatua kero za wananchi.

Katika kuhakikisha kuwa kero hizo zinamalizwa, mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya chama tawala CCM wilaya ya Kinondoni Lucas Mgonja amesema hivi sasa chama hicho kinajipanga kurejesha jimbo hilo pamoja na mengine yote katika mkoa wa Dar es Salaam, ambayo kwa sasa yapo chini ya upinzani.