Kauli ya Rais, kiongozi wa dini kuwa mwanasiasa

Alhamisi , 8th Jul , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa wakati mwingine dini na siasa vinaendana lakini pia wakati mwingine ni vitu vivyokinzana ambapo amesisitiza kwamba vyote hivyo vinatakiwa kutazamwa kwa umakini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Julai 8, 2021, mkoani Morogoro aliposhiriki Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili mkoani humo aliyoianza hapo jana akitokea Jijini Dodoma.

"Ndugu zangu niseme, wakati mwingine dini na siasa ni vitu vinavyokwenda sambamba lakini wakati mwingine ni vitu vinavyokinzana, inategemea mtu anaitumiaje, si vibaya kiongozi wa dini kuwa mwanasiasa, lakini kuna ubaya anapoitumia dini ile kufanya siasa, ndugu zangu yote hayo inabidi tuyatazame kwa umakini," amesema Rais Samia.