
Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amesoma jina hilo ambalo lilifungwa ndani ya bahasha 3 iliyotoka kwa Rais mbele ya wabunge wa bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Mimi Rais John Pombe Magufuli, kwa mamlaka niliyonayo namteua Ndg. Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, alisikika Spika Ndugai alipokuwa akisoma barua hiyo yenye jina la waziri mkuu.
Kwa mujibu wa katiba, Bunge limethibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu huyo Mhe. Kassim Majaliwa kwa kura 258 za ndio, sawa na asilimia 73.5.
Kassim Majaliwa aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ukuu wa wilaya na naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).