Ijumaa , 23rd Jan , 2015

Taasisi ya utafiti wa namna ya kupunguza umaskini nchini Tanzania - REPOA kiasi cha pesa kinachotolewa na serikali kwa taasisi zinazohusika na utafiti wa sera za uchumi na maendeleo bado ni kidogo kulinganisha na mahitaji

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa REPOA Profesa Samuel Wangwe

Taasisi ya utafiti wa namna ya kupunguza umaskini nchini Tanzania - REPOA imesema kiasi kidogo cha pesa kinachotolewa na serikali kwa taasisi zinazohusika na utafiti wa sera za uchumi na maendeleo kuwa ni moja ya sababu zinazochangia kasi ndogo katika harakati za kupunguza umaskini.

Mkurugenzi Mkuu wa REPOA Profesa Samuel Wangwe, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa orodha ya taasisi za utafiti wa sera duniani, chanzo cha ufadhili wa fedha kwa taasisi hizo na mchango wake katika upatikanaji wa sera bora.

Profesa Wangwe, amesema hali hiyo imechangia kuwepo kwa sera za uchumi zisizoendana na mahitaji ya nchi, ambapo ametolea mfano wa Kenya ambako kutokana na ufadhili mzuri wa fedha kutoka serikalini, taasisi yake ya utafiti ya KIPRA imeibuka kuwa taasisi bora ya utafiti wa sera kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara