Jumatatu , 6th Jun , 2016

Waziri wa ujenzi ,uchukuzi na Mwasiliano Prof Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa kampuni za simu nchini zilizoingia makubaliano na serikali kupeleka huduma za mawasiliano vijijini kukamilisha kazi hiyo vinginevyo watachukua hatua kali za kisheria.

Waziri wa ujenzi ,uchukuzi na Mwasiliano Prof Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa kampuni za simu nchini zilizoingia makubaliano na serikali kupeleka huduma za mawasiliano vijijini kukamilisha kazi hiyo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Prf Mbarawa ametoa kauli hiyo mjini Iringa mara baada ya kukagua miundombinu ya kampuni ya simu ya TTCL na kubaini kuwa bado kuna baadhi ya vijiji havijafikuiwa na huduma ya mawasiliano licha ya mkataba wa kutekeleza kazi hiyo kati ya serikali na kampuni hizo kusainiwa miaka miwili iliyopita.

Kuhusu suala la kukatwa kwa mkongo wa taifa katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Iringa Prf Mbarawa amesema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu yoyote au shirika litakalobainika kuharibu miundombinu hiyo.

Katika hatua nyingine waziri amekagua barabara ya Iringa- Kalenga mpaka hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye urefu wa kma 134 ambayo usanifu wake umeakamilika na kusisitiza kluwa itajengwa kwa kiwango cha lami.