Alhamisi , 10th Nov , 2016

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amezindua kampeni ya mwezi mmoja ya Maadili na Haki za Binadamu.

Mhe. Angella Kairuki, Waziri wa Utumishi na Utawala Bora

Kampeni hiyo itaendeshwa na Taasisi za Takukuru, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mamlaka ya Manunuzi ya Umma pamoja na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Kampeni hiyo inalenga kuhakikisha kuwa taasisi zote za umma na binafsi nchini zinazingatia na kujenga maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa ili kujenga usawa miongoni mwa wanajamii ambapo. Mhe. Kairuki amesema wananchi pia watapewa elimu ya kutambua haki zao na kutoa malalamiko yao.

Valentino Mlowola

Akiongea katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Bwana Valentino Mlowola amekiri kuwepo kwa tatizo la vitendo vya rushwa ambayo amesema kwa hapa nchini ni tatizo kubwa na kuelezea namna ambavyo wamejipanga kumaliza tatizo la rushwa nchini.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Bahame Tom Nyanduga amesema nilazima viongozi watimize wajibu wao kwa kuzingatia utawala bora na haki za binadamu.