
Akiongea mara baada ya kukamilika kwa kazi ya kuwasilishwa kwa taarifa za kamati hizo Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta amesema mjadala utaanza leo saa kumi, ambapo jumla ya wajumbe 26 watapata fursa ya kujadili.
Mhe. Sitta amesema utaratibu wa mjadala wa sura hizo mbili ya kwanza na ya sita, umepangwa kwa kuzingatia kuwa mjadala huo unatoa fursa kwa wastani wa wajumbe 50 wa Bunge Maalum la Katiba kujadili kila siku.