
Mjumbe wa kamati ya Tanzania kwanza nje ya bunge, msanii Steve Nyerere.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar-es-Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Agustino Matefu na mjumbe wa kamati Bw. Steve Nyerere wamesema mikutano hiyo itaanza tarehe 17 mwezi huu huko
Kibanda Maiti na Chake Chake na pia watatumia mikutano hiyo ya hadhara kuwahamasisha kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kurudi katika bunge maalum la Katiba ili kuwapatia wananchi katiba iliyo bora.
Kamati hiyo ya Tanzania kwanza inaundwa na vijana wenye taaluma mbali mbali wakiwemo wasanii ambapo ina lenga kuhakikisha suala la amani ya nchi linaendelezwa na kufanywa kuwa ni ajenda ya kwa mwananchi wa Tanzania.