Mchuuzi wa Samaki akiwa sokoni
Kamati hiyo ndio jukwaa pekee la kimataifa ambapo wadau wa kimataifa wa uvuvi wanakutana kujadili matatizo, changamoto na masuala ya uvuvi na kutoka na mapendekezo ya jinsi ya kushughulikia changamoto hizo.
Kikao hicho kimewaleta pamoja wawakilishi wa serikali, mashirika ya kikanda ya uvuvi, asasi za kiraia, wavuvi, jumuiya ya kimataifa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya FAO, la mpango wa chakula duniani WFP na IFAD.
Katika kikao hicho sula kubwa linalojadiliwa ni uvuvi haramu na njia za kukabiliana nao, ambao kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa FAO Graziano da Silva umeongezeka na unatia hasara kubwa, lakini mkataba wa uvuvi ulioanza kutekelezwa karibuni amesema utakabiliana na changamoto hiyo.




