Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ndani ya chama hicho, kikao hicho cha dharura pamoja na mambo mengine kitajadili hali ya mwenendo wa siasa nchini.
Katika kikao hicho cha siku mbili, Kamati Kuu pia itapokea taarifa na kujadili kabla ya kufanya maamuzi kuhusu mipango mbalimbali inayoendelea ya kukipanga chama ili kiendelee kufanya shughuli zake kwa ufanisi.
Pia kupanga mikakati ya kuimarisha misingi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kufikia nchi nzima, kupitia usimamizi wa kanda 10 za chama.




