Jumatano , 2nd Jul , 2014

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania leo imepokea taarifa kutoka ub

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Kamilius Membe.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania leo imepokea taarifa kutoka ubalozi wa Libya nchini ikieleza kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya Bw. Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.

Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Libya ambapo imeelezwa kuwa marehemu alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.

Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini na kuamua kumkimkimbiza hospitali ya AMI iliyopo Oysterbay ambako alitangazwa kuwa amekwisha fariki duni, kifo ambacho kimethbitishwa pia na jeshi la polisi Jijini Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu Nwairat umehamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili na kwa sasa ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wake kwenda nchini Libya kwa mazishi. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya ushirikiano wake katika kipindi hiki kigumu.