Ijumaa , 17th Mar , 2023

Wakati Taifa la Tanzania leo Machi 17/2023 likiadhimisha miaka miwili ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli, Kadinali mstaafu Polykarp Pengo amezuru wilayani Chato kwa ajili ya kutembelea kaburi la Hayati Magufuli

Akizungumuza na waandishi wa habari akiwa ofisi ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Kardinali Pengo alisema amefanya hivo kwani hakupata fursa hiyo wakati wa mazishi ya Dk Magufuli

“Nimechukua nafasi hii kwenda kutoa heshima kule Chato, kwenye kaburi la yeye aliyezoea kuniita mimi baba yake, mimi nilipenda zaidi kumuita zaidi rafiki yangu, Dk John Pombe Magufuli

“Sikuweza kufika wakati ule wa mazishi, kwa sababu hali yangu ya afya haikuwa nzuri, na nilipoweka dhana kujaribu kufika kwenye mazishi, niliambiwa tu na madaktari kwamba wewe unataka kuleta msiba juu ya msiba. amesema Pengo