Jumatano , 17th Feb , 2016

Muungano wa Afrika(AU), Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya(EU) na shirika la kimataifa la wazungumzaji wa Kifaransa(IOF) wanafuatilia kwa karibu hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC hususani kwa mtazamo wa chaguzi zijazo nchini humo.

Siku ya uchaguzi mwaka 2011 Bunia, DRC.

Mashirika hayo manne yanasisitiza umuhimu wa chaguzi hizo ambapo kufanyika kwake kwa amani, uhuru, uwazi , utulivu na kwa wakati kutachangia kiasi kikubwa hatua zilizopigwa nchini DRC kwa zaidi ya muongo mmoja.

Masharika hayo yamewataka wadau wote wa kisiasa nchini Congo kutopoteza fursa ya kuhakikisha wanafanikiwa kuendesha chaguzi hizo , kudumisha amani na demokrasia, ikiwemo kupitia mchakato wa kisiasa.

Mashirika hayo manne yamesisitiza umuhimu wa mjadiliano na kusaka muafaka baina ya wadau wa kisiasa kwa kuzingatia na kuheshimu demokrasia na utawala wa sheria.