Ijumaa , 28th Mar , 2014

Jukwaa la Katiba nchini Tanzania limekemea juu ya uwepo wa taarifa za vitisho kwa waandishi wa habari ambao hutakiwa kutoandika mabaya yanayoendelea ndani ya bunge maalum la Katiba.

Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Hebron Mwakagenda.

Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bw. Hebron Mwakagenda, ametoa kauli hiyo na kuongeza kuwa baadhi ya vyombo vya habari vimeanza kuandika habari nyepesi ambazo amesema haziibui ukweli wa yale yanayotokea ndani ya bunge hilo.

Mwakagenda ameviomba vyombo vya habari kutambua jukumu walilonalo la kuwataarifu Watanzania kuhusu mchakato wa katiba mpya na hivyo wasikatishwe tamaa na vitisho hivyo ambavyo kimsingi ameviita ni vya watu wanaolenga kukamwisha upatikanaji wa katiba mpya.