Alhamisi , 21st Jul , 2016

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Jakaya Mrisho Kikwete amewatumia salamu wale wote ambao waliandaa Rambirambi wakidai kuwa chama hicho kitakufa.

Dkt Jakaya Kikwete (Kushoto), na Katibu wa CCM Abdulrahman Kinana katika kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho

Kikwete ambaye ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akifungua kikao cha kamati kuu ya CCM Taifa kilichokuwa na ajenda ya kumpendekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho.

Pamoja na kuzungumzia nafasi yake ya uenyekiti kwa cha miaka 10, Kikwete amesema kuwa waliokuwa wanajiandaa na salamu za rambirambu hawata fanikiwa kwani CCM iko palepale.

Rais John Magufuli anatarajiwa kupigiwa kura katika Mkutano Mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mjini Dodoma.