Ijumaa , 26th Dec , 2014

Serikali Wilayani Butiama Mkoani Mara imesema ni dhana potofu ulihusisha jeshi la Mgambo na Chama Cha Mapinduzi CCM, kama kauli za baadhi ya watu wanavyochochea vijana kutojiunga na mafunzo ya jeshi hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara Bi Angelina Mabula.

Mkuu wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara Bi Angelina Mabula, ametoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya Mgambo katika kijiji cha Bisarya Wilayani humo, ambapo amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa vijana ili kuwajengea uzalendo kwa taifa lao,

Naye Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini Meja Jenerali Raphael Muhuga,amesema mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa nchini kote na kuwataka wananchi kutohusisha jeshi hilo na Chama chochote cha siasa.

Naye mshauri wa Mgambo wa wilaya ya Butiama afisa mteule daraja la pili wa jeshi la wananchi Isaya Mkachimwa,akitoa taarifa katika kuhitimisha mafunzo hayo, amesema vijana 180 wamefanya vizuri katika mafunzo hayo ambayo yamehusisha usalama wa raia, kupambana na kuzuia vitendo vya rushwa pamoja na kuokoa watu na mali wakati wa majanga huku mmoja ya wahitimu akiomba serikali kuwapa kipaumbele katika ajira kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.