Alhamisi , 22nd Mei , 2014

Mkuu wa mkoa wa Kiigoma Luten Kanal mstaafu Issa Machibya amewataka wananchi kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa wazee, ambavyo vimekuwa vikifanyika katika jamii na kusababisha vifo na wengine kuwa ombaomba.

Mkuu wa mkoa wa Kiigoma Luten Kanal mstaafu Issa Machibya

Mkuu wa mkoa wa Kiigoma Luten Kanal mstaafu Issa Machibya amewataka wananchi kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa wazee, ambavyo vimekuwa vikifanyika katika jamii na kusababisha vifo na wengine kuwa ombaomba.

Luten Kanal Mstaafu Machibya ametoa wito huo wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo ya asasi bora zaidi Tanzania kwa chama cha kusaidia wazee Kasulu, ambapo amesema vitendo vya mauaji na huduma zisizoridhisha kwa wazee havikubaliki na kwamba ni wajibu wa jamii na wadau wengine kusaidia ustawi wa wazee kwa kuweka mifumo itakayoweza kuwasaidia kupata mahitaji ya msingi ikiwa ni pamoja na malazi, mavazi, chakula na matibabu.
 
Kwa upande wake katibu mtendaji wa chama cha kusaidia wazee Kasulu SUWATA Cotrida Kokupima, amesema chama hicho kimeanza kutoa elimu katika vijiji 14 wilayani humo baada ya utafiti kuonesha kuwa wazee wengi hasa vijijini wametelekezwa, na wanakabiliwa na umasikini uliotopea unaopelekea kutopata huduma za msingi ikiwa ni pamoja na matibabu huku mkuu wa wilaya ya Kasulu Dahn Makanga akiiagiza idara ya afya wilayani humo kuhakikisha wazee wanatibiwa bure vijijini.