
Jaji Warioba walijikuta akikatizwa mara kwa mara kusoma taarifa yake kutokana na wajumbe kupiga makofi na kushangilia kwa nguvu wakati akianisha mambo mbalimbali na maoni ya wananchi kuhusu aina ya muundo wa muungano wanaoutaka pamoja na kueleza jinsi Tanganyika ilivyovaa koti la muungano.
Amesema kuwa kimsingi hatuwezi kuendelea na muungano huu, kwani si ule tena tulioachwa na waasisi wetu ambao ulikuwa wa serikali mbili nchi moja, wakati sasa tuna nchi mbili serikali mbili jambo ambalo linatulazimu kuwa na muundo wa muungano wa serikali tatu .