Jumamosi , 18th Nov , 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.Selemani Jafo ametoa wito wa kulinda na kuhifadhi mazingira ya Ziwa  Tanganyika na rasilimali zake ili liendelee kuinufaisha jamii na kuleta maendeleo endelevu.

Dkt. Jafo akifungua Mkutano wa 11 wa Mawaziri wa
Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mulungushi jijini Lusaka, Zambia Novemba 17, 2023.

Amesema ni wajibu wetu kuhakikisha changamoto zinazolikabili zikiwemo kupungua kwa kina cha maji, uchafuzi wa mazingira kutoka viwandani na majumbani, upotevu wa bayoanuai na mchanga zinakwisha.

Dkt. Jafo ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa 11 wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mulungushi jijini Lusaka, Zambia Novemba 17, 2023.

Dkt. Jafo amesema ziwa hilo ni urithi wa shughuli za kiuchumi na kijamii zinazofanywa ndani ya bonde zikiwemo uvuvi, kilimo, ufugaji, makazi ya watu na uchimbaji madini.

“Tutambue kuwa Ziwa Tanganyika ni zaidi ya kapu la chakula kwa jamii zetu na bonde lake ni nyumbani kwa zaidi ya watu milioni 13, ni eneo bora kwa kuunganisha nchi zetu nne zinazolizunguka, hivyo hatuna budi kushirikiana