Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Robert Salim
Akizungumza Mkoani humo katika uzinduzi wa huduma ya Madaktari bingwa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Robert Salim amesema kuwa hivi sasa Mkoa huo una Madaktari bingwa watano wakati mahitaji ya Mkoa huo ni Madaktari 20.
Dkt. Salim amesema kuwa Madaktari wanaohitajika ni pamoja na Daktari wa Virgiatrition,daktari wa watoto,daktari wa magonjwa ya afya ya akili,magonjwa ya Moyo, Daktari anayehusika na magonjwa ya njia za mkojo,pamoja na madaktari macho,pua na masikio.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa matibabu na huduma za kiufundi kutoka (NHIF), Dkt. Frank Lekey, amesema pamoja na kutoa huduma madaktari hao watabadilishana ujuzi na madaktari hao waliopo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Wanguvu amesema kuwa ujio wa madaktari hao ni ukombozi wa wananchi wengi ambao walipewa rufaa ya kwenda kutibiwa Muhimbili lakini walikosa nauli ya kwenda kupata matibabu hayo.
Nae Mganga Mkuu wa Serikali, Mohammed Bakari amezitaka Hospitali zote nchini kutoka kipaumbele katika matibabu ya wazee ili wasione wametengwa na jamii inayowazunguka baada ya kulitumikia taifa katika ujana wao.