Jumatano , 15th Jun , 2016

Wakati Tanzania itaungana na nchi nyingine za Africa kuhadhimisha siku ya Mtoto wa Africa hapo kesho , Halmashauri ya wilaya ya Ilala inakabiliwa na changamoto kubwa ya ubakaji kwa watoto.

Wakati Tanzania itaungana na nchi nyingine za Africa kuhadhimisha siku ya Mtoto wa Africa hapo kesho , Halmashauri ya wilaya ya Ilala inakabiliwa na changamoto kubwa ya ubakaji kwa watoto.

Afisa Habari wa Manispaa ya Wilaya ya Ilala Bi Tabu Shaibu amesema kuwa kuanzia mwaka 2013 jumla ya matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto yapatao 1213 yameripotiwa katika kituo cha Amana Hospitali huku matukio ya ubakaji yakiwa 469 yakifuatiwa na matukio ya kulawitiwa.

Aidha Manispaa inatoa wito kwa jamii kutoa taarifa na kufika katika vituo vya huduma ikitokea kuna ukatili wa kijinsia umejitokeza lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa matukio kama hayo yanatokomezwa kabisa.