Jumatatu , 18th Oct , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa ukorofi na kukosekana kwa nidhamu ndiyo kulikopelekea kumhamisha tena kwa kumhurumia aliyekuwa Mkurugenzi wa wilaya ya Longido Juma Mhina, ili akajifunze.

Juma Mhina, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 18, 2021, wakati akizungumza na wananchi wa Longido, ambapo amewasisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa nidhamu na kusema kwamba asingemhurumia asingemteua tena.

"Longido hapa kulikuwa na mkurugenzi mkorofi sana, hakukuwa na nidhamu ya kufanya kazi ndiyo maana nikamtoa nikampeleka sehemu nyingine akajifunze na hilo ni kumhurumia ilikuwa nimuache kabisa," amesema Rais Samia