Alhamisi , 1st Dec , 2022

Watu watatu wanashikiliwa Jijini Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mhadhili wa chuo kikuu cha SAUT jijini Mwanza Hamida Musa  anayedaiwa kuuawa kwa kunyongwa na mtandio 

Wanaoshikiliwa ni mfanyakazi wake wa ndani (House Girl), Mama wa mfanyakazi huyo pamoja na ndugu mmoja wa mfanyakazi huyo

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema watu hao wanahojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani

Polisi wamesema katika msako wamemkuta mfanyakazi huyo wa ndani akiwa na vitu mbalimbali vya marehemu ikiwemo hereni, pete na vitu vingine vya thamani

Mwili wa Hamida ulikutwa Jumanne Novemba 29, 2022 nyumbani kwake Mtaa wa Buzuruga Mashariki wilayani Ilemela mkoani Mwanza ukiwa umelala sakafuni kifudifudi ukiwa na mtandio shingoni mwake huku mfanyakazi wake wa ndani ambaye alikuwa akiishi hapo akiwa ametoweka