Katika hotuba yake ya kwanza, Sunak amesema kwamba Uingereza kwa sasa inakabiliwa na mdororo mkubwa wa kiuchumi na kwamba amechaguliwa na wabunge wa chama chake ili kurekebisha makosa ya mtangulizi wake aliyejiuzulu Bi.Liz Truss.
Lingine linalojiri ni kuunda upya baraza la mawaziri huku vigogo kadhaa wakitupwa nje na wengine wakijiuzulu, Jacob Rees-Mogg,mmoja wa watiifu wakubwa wa Boris Johnson amejiuzulu wadhifa wake kama katibu wa fedha, huku Brandon Lewis akijiuzulu kama katibu wa sheria.
Katika hotuba yake ya awali, Liz Truss alitetea maamuzi yake ya kupunguza kodi na kwamba mtu anayekua kiongozi anatakiwa awe na maamuzi magumu.
Rishi Sunak mwenye miaka 42, anakuwa ni Waziri Mkuu mdogo zaidi katika kipindi cha miaka 200.
Sunak alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama mbunge mnamo mwaka 2015 na katika kipindi cha miaka miwili ya ubunge mpango wa Brexit ulikuwa umeshika kasi ambapo yeye aliunga mkono Uingereza kuondoka EU wakati wa kura ya maoni mwaka 2016.