Jumatatu , 18th Jul , 2016

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi ametangaza azma ya kuwa chukulia hatua wale wote ambao wamehusika kuhujumu mradi wa wodi 7 za wazazi zilizokuwa chini ya mradi wa TASAF kwa ufadhili wa benki ya dunia uliogarimu shilingi Milioni 500 ambazo

serikali inalipia deni lake hadi hizi sasa.

Mkuu wa wilaya hiyo Mhe Ally Hapi amesema hayo jijini Dar es salaam katika mkutano na viongozi mbalimbali wa manispaa hiyo, waganga wakuu wa vituo vyote vya afya, Zahanati na Hosptali za wilaya hiyo kwa lengo la kupeana mikakati ya kuboresha mazingira ya vituo vya kutolea huduma za afya.

Mhe. Hapi amesema imesikitishwa na ufisadi huo ambayo deni lake linalipwa kodi za wananchi huku majengo yaliyojengwa na fedha hizo yakiwa hayatumiki na mengine yakiwa yamebomoka bila kuanza kutumika.

Hapi amewataka wale wote ambao wanajua wamehusika katika kuhujumu vityuo vya afya, kutowalipa madaktari posho zao sambamba na kutumia madaraka yao vibaya waache mara moja kwani uongozi wa awamu hii autamvumilia mtu yeyote asiye mwadilifu.

Akiongelea ukaguzi alioufanya katika vituo vya afya wilayani humo, Ally Hapi amebaini kuwepo kwa msongamano wa wagonjwa, upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo, dawa na vifaa tiba, upungufu wa wahudumu wa afya na kukosekana kwa hati ya umiliki wa viwanja katika vituo vingi vya wilaya hiyo.

“Idadi ya wakazi wa Kinondoni inakadiriwa kuwa Milioni mbili na laki moja na nusu hivi sasa, vituo vya afya vimelemewa ni lazima tutumie mbinu zote kuhakikisha tunakabilia na haliilivyo, tutajenga jengo lingine katika kituo cha afya Kijitonyama kukabiliana na msongamano na kuongez jengo lingine Mwananyamala Hosptali” amesema Hapi

Katika hatua nyingine Mhe. Hapi amesema wilaya yake itatoa zawadi mbalimbali kwa madaktari na wauguzi watakao fanya kazi kwa bidii, ikiwa nipamoja na Kutolalamikiwa na wagonjwa, aliye vuka lengo la idadi ya wagonjwa anaopaswa kuwahudumia.

Vigezo vingine vyitakavyopelekea muuguzi kupewa zawadi nipamoja na ubunifu na kusaidia kuboresha huduma katika kituo chake, atakaye zingatia sheria na utaratibu kwa kiwango cha juu, atakaye onyesha kuoka maisha kwa kiwango cha dharura na wanaofanya kazi bila kulalamika hata katika muda wa ziada.