Jumamosi , 15th Mei , 2021

Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo aliyekuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Salum Hamduni, kuwa Kamishna wa Polisi (CP).

Kushoto ni Salum Hamduni aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU pamoja na Kamishna wa Polisi na kulia ni Sylvester Mwakitalu, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)

Mbali na kumpandisha cheo, pia amemteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), akichukua na nafasi ya Brigedia Jenerali John Mbungo ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Aidha, Rais Samia pia, amemteua Sylvester Mwakitalu, kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Biswalo Mganga, ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Ikumbukwe kuwa CP Hamduni, aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Ilala, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro na Arusha.