Jumanne , 24th Oct , 2023

Shirika la msalaba mwekundu linalohusika na utoaji wa huduma ya kwanza limethibitisha taarifa za mateka wawili wa Israel kuachiwa huru na kundi la Hamas na kuwatoa nje ya Ukanda wa Gaza 

Taarifa  ya DW imesema kundi la Hamas limewaachia huru wafungwa wawili wanawake kwa sababu za kibinadamu.

“Wanawake wawili wa Israel walioachiliwa na kundi hilo wamekabidhibiwa kwa jeshi la Israel na wamepelekwa katika kituo cha afya nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya waziri mkuu wa Israel wanawake hao ni Nurit Cooper, mwenye umri wa miaka 79 na Yocheved Lifshitz wa umri wa miaka 85,”imesema taarifa hiyo.