Alhamisi , 29th Sep , 2022

Kampeni ya Mama lishe wa thamani imefikia tamati kwa mkoa wa Dar es Salaam katika wilaya zake zote tano ambazo ni Kinondoni, Temeke, Kigamboni, Ubungo na Ilala, ambapo hii leo imempata mpishi hodari wa half cake ndani ya wilaya ya Ilala na kupatiwa zawadi ya kiwanja.

Veronica Kakobe kulia, akipatiwa zawadi kutoka Poa Supermarket baada ya kushinda

Awali katika shindano la kumsaka Mamalishe wa thamani lilianzia Temeke kumpata mkali wa chapati, kisha Kigamboni kumpata hodari wa kalmati, kindoni kumpata hodari wa maandazi, Ubungo kumpata hodari wa donati, na hatimaye hodari wa half cake Ilala nzima akapatikana.

Akizungumza mara baada ya kuibuka mshindi na kuzawadiwa zawadi ya kiwanja kutoka Mwendapole CO.LTD pamoja na zawadi mbalimbali ikiwemo sukari na mafuta, na kushukuru kwa nafasi hiyo huku akiwaomba wanawake wengine kujitokeza wanaposikia fursa za namna hiyo

Kwa upande wao baadhi ya wadhamini wa shindano hilo, wamjivunia kuwa sehemu ya shindano hilo, kwani wameyaona manufaa na umuhimu katika kuwainua na kuwaendeleza wanawake kiuchumi.

Shindano Mama Lishe wa thamani litaifikia mikoa mbalimbali nchini na je ungependa tuanze na mkoa gani baada ya Dar es Salaam?, tuandikie maoni yako ya mkoa unaotaka tuanze kupitia mitandao yetu ya kijamii ya East Africa Radio na utuambie ni kitafunwa gani kinapendwa kwenye huo mkoa.