
Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume.
Fatma Karume ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv kuwa mfuasi wa chama chochote cha siasa nchini, kutokana na historia ya baba yake mzazi kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi huku yeye akionekana kuwa karibu sana na viongozi wa vyama vya upinzani.
Fatma Karume amesema "sijawahi kumiliki na wala sitaki kumiliki kadi ya chama chochote, kuhusu kushiriki kwenye siasa naweza kushiriki bila kuwa mwanachama wa chama chochote, kwani sasa hivi nawakosoa vizuri sana kwa hiyo naweza kutoa maoni yangu hata kama wakiniita mwanaharakati." amesema Fatma Karume.
"Kuhusu kuwa mfuasi wa chama cha siasa kwa sasa nikitaka nitafanya nisipotaka nitaacha, nitawaambia nikimiliki kadi ya chama chochote." ameongeza Fatma Karume.
Hivi karibuni akizungumzia kuonekana kwake kwenye maazimio ya vyama vya upinzani nchini Fatma Karume alisema alionekana kwenye mkutano huo baada ya kualikwa na vyama husika kutoa elimu juu ya masuala ya katiba.