Dkt. Kanyaro amebainisha hayo kupitia kipindi cha Supamix kinachorushwa kupitia East Africa Radio baada ya kuwepo wimbo kubwa la watu kupata ugonjwa huo, huku wengine wakidhani unatokana na magonjwa ya kurithi kifamilia kama yalivyo mengine yanayojulikana.
"Shinikizo la jicho au presha ya jicho ni moja kati ya magonjwa yanayoleta upovu wa kudumu. Hili tatizo linawaathiri watu wote nikiwa namaanisha kwamba mtoto anaweza akazaliwa nalo kama ile sehemu yake ya kutolea machozi haitakuwa vizuri. Tunasisitiza sana jamii kufahamu ugonjwa huu wa presha ya macho ni lazima upime", amesema Dkt. Kanyaro.
Mtazame hapa chini Dkt. Neema Kanyaro akieleezea vizuri jinsi unavyotokana ugonjwa wa Presha ya macho na sababu zake nyingine.






