Balozi wa Tanzania Ufaransa - Begum Karim-Taj
Akihutubia kikao cha ngazi ya mawaziri kwenye mkutano huo wa COP21, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Begum Karim Taj amesema kiwango hicho kitasaidia harakati ambazo tayari nchi hiyo imeanza kuchukua kukabiliana na mabadiliko hayo, ikiwemo matumizi ya nishati endelevu kama vile gesi asilia na joto ardhi.
Baada ya hotuba hiyo, Balozi Begum amesema pamoja na mahitaji ya fedha hizo suala ni uwazi na upatikanaji wa fedha hizo kwa kuwa mara nyingi fedha hizo zinaahidiwa na hazifiki na kutumika kwa uwazi.
Aidha bi. Bigum amesema kuna tatizo katika upatikanaji wa fedha hizo na uwazi wa upatikanaji kwa kuwa kuna uwezekano wa kuahidiwa na kuambiwa fedha zimetoka lakini zimetokaje suala hilo ndio huwa linakua kizungumkuti.