Ijumaa , 4th Mar , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa ameziagiza halmashauri zote za mkoa wa Dodoma kuchagua zao la biashara la kulima ili kuwawezesha wananchi kuinuka kiuchumi na kukabiliana na baa la njaa ambalo huukumba mkoa huo kila mwaka.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa.

Gallawa ametoa agizo hilo mjini Dodoma wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Dodoma katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM makao makuu.

Amesema kuwa wilaya ya Kondoa imejipanga kulima zao la muhogo ambapo halmashauri ya wilaya hiyo imeweka mkakati mzuri wa zao hilo na kwamba serikali ya mkoa imejipanga kutafuta soko la zao hilo katika viwanda mbalimbali.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa wameandaa mkutano mkubwa wa uwekezaji ambao utauwezesha mkoa wa Dodoma kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa huu ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha za kuwezesha mkutano huu.