Jumapili , 25th Jul , 2021

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, amemuagiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Festo Dugange kuchunguza mwenendo wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Hamis Dambaya kutokana na upotevu mkubwa wa fedha,

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Hamis Dambaya (kulia).

kwenye ujenzi wa mradi wa stendi ya Mabasi ya Mangaka.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maagizo hayo Julai 24, 2021 alipofanya ziara ya kustukiza katika stendi ya Mabasi ya Mangaka iliyopo Wilaya ya Nanyumbu na kukasirishwa na uongozi wa Wilaya kwa kufanya upotevu mkubwa wa fedha usiolingana na matokeo ya ujenzi wa mradi huo.

Ujenzi wa majengo ya stendi hiyo umetumia shilingi bilioni 2.2 kiasi ambacho Makamu wa Rais amesema hakilingani na ujenzi huo na ameagiza kupelekewa taarifa hizo ofisi kwake haraka iwezekanavyo.

Amesema viongozi hawana budi kusimamia fedha za serikali zinazopelekwa katika maeneo yao ili kuwaletea maendeleo wananchi.