
Patrobasi Katambi ametoa ahadi hiyo jijini Dodoma wakati wa harambee maalum ya kuhamasisha uchangiaji wa taulo za kike, harambee iliyoandaliwa na EAST AFRICA TV Limited.
Katambi amesema kuwa, "katika kuunga mkono kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na kituo cha EATV/EARADIO kwa Mkoa wetu wa Dodoma tumeamua kuungana na wadau mbalimbali wa maendeleo kuchangia taulo za kike ambazo ni msaada mkubwa kwa mabinti zetu ambao wanakosa masomo pindi wanapokua katika siku za hedhi."
"Changamoto inayowakuta watoto wa kike ni hasara kubwa kwa kizazi cha sasa na baadae hivyo tumeona ni vyema pia kuwashirikisha watu mbalimbali katika kitoa msaada huo kwa wadogo zetu ili kuleta mapinduzi katika sekta ya elimu nchini.", amesema Katambi.
Kwa mwaka 2019 Kampeni ya Namthamini imelenga kuwasaidia takribani watoto wakike 5000 waliokuwa mashuleni ambao wamekuwa wakikosa masomo kwa taribani siku 30 kwa mwaka.