Jumamosi , 24th Mei , 2014

Mkemia mkuu wa serikali Profesa Samwel Manyele ameomba wananchi kufichua uhalifu wa matukio ya sumu zinazotokana na kemikali kwa ajili ya kukomesha matukio hayo hapa nchini.

Mkemia Mkuu wa serikali, Prof Samwel Manyele

Mkemia mkuu wa serikali Profesa Samwel Manyele amesema wakati mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Rukwa na Mbeya ikiongoza kuwa na matukio ya sumu zinazotokana na kemikali, ameomba wananchi na wadau wengine waendelee kufichua uhalifu huo kwa ajili ya kukomesha matukio hayo hapa nchini.

Profesa Manyele amesema hayo mkoani Mbeya wakati akizungumza na wakurugunzi wa viwanda, migodi, na wanaoendesha shughuli zinazotumia kemikali, amesema juhudi za pamoja zinahitajika ili kuokoa maisha ya wananchi, ambao wengi hawana uelewa wa matumizi ya kemikali hizo hatari na zinazopoteza maisha ya watu:

Baadhi ya wamiliki wa viwanda na shughuli zinazotegemea kemikali wamesema kuwa wananchi wengi wanaodhurika na kemikali hizo ni wale waliokosa ufahamu ambao baadhi yao ni rahisi kurubuniwa na kutoa kemikali hizo kwa watu ambao wanaokwenda kufanyia vitendo vya uhalifu: