Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam waziri wa wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu amesema kutokana na hali hiyo wizara imepiga marufuku matumizi ya vilainishi vinavyotumiwa na baadhi ya makundi yanayo jihusisha na vitendo hivyo.
Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa serikali imeamua kuzuia vilainishi hivyo kwani vimetajwa kuchochea vitendo hivyo ambavyo nikinyume na sheria na taratibu za nchi nakuongeza kuwa vitendo hivyo nimiongoni mwa sababu inayochangia ongezeko la VVU.
Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa kwa sasa serikali inajikita kuhakikisha kuwa inajengo wodi za wazai, kununua vifaa tiba, madawa ya kutosha katika hosptali zake na sio ununuzi wa vilainishi hivyo.





