Kituo cha Gerezani
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya DART iliyotolewa jana Februari 7, ujenzi huo utahusisha barabara ya Kilwa kuanzia katikati ya Jiji la Dar es salaam hadi Mbagala Rangi Tatu na barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni, Barabara ya Chang'ombe, Mgulani hadi makutano ya barabara ya Kilwa na eneo la Mgulani JKT.
Aidha katika hatua nyingine, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, imetoa utaratibu utakaotumika kwa safari za daladala zilizokuwa ziantumia kituo hicho, kama inavyoonekana hapo chini.