
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Stella Manyanya
Amevipongeza Viwanda vyote kwa kwa kuendele kuzalisha ndoo na Vifaa vingine kwa wingi vinavyotumika kunawia mikono ambavyo vinahitajika sana katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya ugojwa wa Corona
“Nawapongeza na nimefurahishwa sana na uzalishaji mzuri na hakuna wasiwasi kwamba tutakuwa na upungufu wa ndoo za kunawia mikono katika maeneo yetu maana nimejionea uzalishaji mkubwa unaoendelea na ambao utaweza kukidhi maahitaji ya watanzania ya upatikanaji wa ndoo za kunawia mikono”
Aidha, ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara wanaendelea kuuza bei Kubwa ndoo na vifaa vingine vya kunawia mokono kwa kufanya mapambano ya ugojwa huu kuwa fursa kwao ya kujinufaisha maradufu na kujipatia kipato kikubwa tofauti na ilivyokuwa awali.
“Natoa onyo kwa wafanyabiashara wote hasa wa reja reja kuna baadhi yao ambao wanatumia muda huu wa mapambano ya Corona kama fursa ya kujinufaisha maradufu, Ni marufuku kwa mtu yeyote kuongeza bei kupita kiasi maana kuna wafanyabishara wanaongeza mara mbili ya bei walizonunulia kiwandani”