Jumatatu , 8th Feb , 2016

Watu sita wanauguza majeraha nchini India baada kushambuliwa wakijaribu kumdhibiti chui aliyekuwa ameingia kwenye shule ya Vibgyor nchini India

Watu hao walikubwa na maswaibu hayo baada ya kujaribu kumzuia chui huyo ndipo alipoanza kuwarukia na kuwauma huku watu wengi wakikimbia kuepuka kadhia hiyo.

Chui huyo mwenye umri wa miaka nane alisumbua eneo hilo kwa muda wa zaidi ya saa nane na baada ya kukamatwa alichomwa sindano na kumfanya atulie na baadae aliachiwa na kurejea porini.

Kwa mujibu wa sensa ya wanyama mwitu iliyofanywa majuzi nchini India inakadiriwa kuwa na idadi ya chui kati ya 12,000 na 14,000.

SOURCE: BBC