Christina ahukumiwa miaka 102 jela

Alhamisi , 8th Jul , 2021

Mwanamama Christina Greer (38) wa Nebraska amehukumiwa kifungo cha miaka 64 hadi 102 kwenda jela kwa unyanyasaji wa kingono ambapo aliyafanya kati ya mwaka 2017 na 2018.

Picha ya Christina Greer

Hukumu hiyo inakuja baada ya Greer kupatikana na hatia ya mashtaka matatu ya unyanyasaji wa kingono uliohusisha watoto wa kiume wawili wenye umri wa miaka 12 na 13 ambapo alitumia pombe na bangi kuwalewesha wakati wa kulala kama maandalizi ya kufanyanao ngono.

Watoto hao walikuwa ni marafiki wa mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 11.