Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe
Kamanda wa Polisi mkoani humo Henry Mwaibambe, ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya uchunguzi wa matukio matatu ya moto yaliyotokea kwa kufululiza shuleni hapo kati ya Julai 5, 6 na 14 mwaka huu, na kudai kuwa wanafunzi wa kutwa wanadai kwamba wenzao wa bweni wamekuwa wakipendelewa hasa kwenye masuala ya chakula.
Kamanda Mwaibambe ameongeza kuwa mbali na matukio ya moto shuleni hapo, shule hiyo pia imekuwa na historia ya kuwa na wanafunzi watukutu, wavuta bangi na waharibifu.