Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Chadema yaliamsha tena!

Alhamisi , 19th Oct , 2017

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka wazi kwamba hakimuhitaji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bw. Christopher Kazeri kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo kwa madai hawana imani naye pia hana sifa kwani anaweza kusababisha umwagikaji wa damu.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka wazi kwamba hakimuhitaji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo kwa madai kwamba hawana imani naye pia hana sifa kwani anaweza kusababisha umwagikaji wa damu. 

Akiitoa taarifa hiyo Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amesema kwamba Mkurugenzi huyo alipoteza sifa za kusimamia uchaguzi tangu Juni, 24 walipokuwa kwenye uchaguzi wa vitongoji na vijiji  kwa kufoji matokeo katika vijiji kadhaa na kuwalazimisha wasimamizi wabadilishe namba kwenye fomu.

Golugwa amesema kwamba vitendo ambavyo Mkurugenzi huyo alivifanya anavitafsiri kama mambo ya kihuni kwani yalipelekea kugombanisha watu ambao ni ndugu hivyo hofu yao ni kwamba anaweza kusababisha umwagikaji damu katika uchaguzi mdogo wa marudiano Arumeru Mashariki.

"Tumeishauri Tume iweze kuwasiliana na mamlaka ya uteuzi kwamba hatumtaki ndg Kazeri awe msimamizi wa uchaguzi huu mdogo Arumeru Mashariki, kwanza aliingilia uchaguzi wa vitongoji na vijiji na kulazimisha kubadilishwa matokeo ambayo yalionyesha Chadema wameshinda, jambo ambalo lilileta ugombanishi kwa wagombea, na hata wagombea wa CCM walikataa matokeo kwa kukubali kwamba walishindwa na hata wasimamizi na askari waliokuwepo hapo walithibitisha kwamba Chadema walikuwa wameshindwa" Golugwa

Ameongeza  "Kama uchaguzi wa vitongoji Mkurugenzi ametumia mabavu na kufanya uhuni ambao tumeumbatanisha kwa Tume, kwenye uchaguzi huu wa madiwani si ataleta hata vifaru au kusababisha umwagaji wa damu? Kwa busara na hekima ya kawaida matendo aliyoyafanya Kazeri hayampi sifa ya kuwa msimamizi.

Hata hivyo Golugwa amefafanua na kusema kwamba wamewasilisha ushahidi wa wagombea wa CCM wakikataa kupokea ushindi huo wa vitongoji kwa madai kwamba hawawez kupokea ushindi wa  mtutu wa bunduki.
 

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Wanachi wa Kata ya Msowero, wakiwa Katika Mkutano wa Hadhara na Mkuu wa Wilaya

Mwenyekiti atiwa mbaroni kwa kuuza mlima, Msowero

Sehemu iliyokumbwa na Mafuriko Kusini mwa Brazil

Wanaokufa kutokana na mafuriko waongezeka Brazil

Baadhi ya Wabunge Wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi

Serikali yashauriwa kuwa bunifu sekta ya usafiri

Baadhi ya Wananchi Wakishudia Ajali Iliyomgonga Mwendesha Bodaboda

Watatu wanusurika kifo, scania ikimgonga bodaboda

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi (kulia) pamoja na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi (kushoto) wakimpatia vifaa kinga mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa madereva bodaboda wa jiji la Arusha.

Bodaboda 200 Jijini Arusha wanolewa na kufundwa

Rajab Abrahaman Abdalah, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga

CCM Tanga yaijibu CHADEMA kuhusu huduma za kijamii

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama

Wazazi simamieni maadili kwa watoto 

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa