Jumapili , 11th Feb , 2018

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo , kimemlalamikia msimamizi wa uchaguzi  jimbo la Kinondoni kwa kudai kuwa  anaashiria kuharibu uchaguzi unaotarajia kufanyika Februari 17,2018 kwa kutowapa viapo mawakala Februari jana kunaashiria njama

za kutaka wasishiriki shughuli za upigaji na kuhesabu kura. 

Malalamiko hayo yametolewa leo na Viongozi wa CHADEMA leo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi mdogo katika jimbo la Kinondoni pamoja  na la Siha na kata tisa. 

Akiyazungumzia malalamiko hayo Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema sheria inataka mawakala wa upigaji kura kula kiapo cha kutunza siri siku saba kabla ya kupiga kura na wanapaswa kupewa kiapo hicho.

"Anayeapisha ndiye anayesaini, hawezi kuapa mbele ya mtu mmoja na kusaini mwingine, kwa kila mwapishaji katika kila kata anakuwa na sababu zake, msimamizi wa uchaguzi anatumika. Kinachoendelea Kinondoni ni tofauti na Siha, kule Siha wameapa jana na kila wakala ameondoka na kiapo chake, sasa sijui sheria inayotumika Siha ni tofauti na inayotumika Kinondoni" Kigaila. 

Aidha Chama hicho  kimedai kuwa hakipo tayari kukubali hila zozote zinazopangwa ili kuharibu uchaguzi huo.