''Chama kimejipanga kikamilifu kuhakikisha maono na matarajio ya Rais Samia Suluhu Hassan yanatekelezwa kikamilifu katika ngazi zote za utawala''
Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma Jumatano, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, amesisitiza kuwa serikali inatarajiwa kufanya kazi kwa kasi mpya na kwa kuzingatia viwango vya juu vya uwajibikaji ili kufikia malengo ya kitaifa.
