Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) Bw. Joseph Butiku.
Bw. Butiku ameyasema hayo jana kwenye mdahalo wa maadili katika kuimarisha amani, umoja haki kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25, ambapo alibainisha kuwa mtandao huo usio na imani na CCM upo tangu mwaka 1990.
Amesema Mwalimu Julius Nyerere aliuruhusu mapema kuondoka CCM mtandao huo lakini walitega na wameendelea kukaa ndani ya chama huku wakikivuruga kwa kutumia agenda ya vijana tangu miaka ya 1990.
Aidha Butiku alimsifia Rais Kikwete kwamba ni mvumilivu kwa kuwa walionunuliwa walithubutu kumzomea lakini alisimamia misimamo yake na kuwezesha kuendesha machakato huo wa uchaguzi kwa usalama.
Kwa upande wake makamu mwenyeketi wa CCM, (BARA) Philip Mangula amesema vyama vyote vimetia saini na kukubaliana kufuata kanuni za maadili wakati wa Uchaguzi.